WATANO WALALAMIKIWA KAMATI YA MAADILI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa
mpira wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika
mtihani wa utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel
Okwi.
Riziki
Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na
Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha
mtihani huo kinyume cha taratibu.
Naye
Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya
usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si
kweli.
Kwa
mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili
ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini
kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.
TWIGA STARS, ZAMBIA KUCHEZA MACHI 2
Mechi
ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2
mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga
Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa
kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage
inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za
bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.
Shepolopolo
iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa
Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa
mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza
ugenini.
Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina
Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma,
Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma
Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness
Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria
Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia
Maarifa na Zena Said.
STAND UNITED YAIKATIA RUFANI KANEMBWA JKT
Stand
United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji
waliosajiliwa katika dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo
iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi
hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari
16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo
Kanembwa JKT iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika
rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT
ilichezesha wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume
na maelekezo kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa
katika dirisha dogo hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji
wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu
Juma, Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji
Ismail, Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David
Sabugowiga.
Dirisha
dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo
Stand United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao
matatu kwa Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali
mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT
kugomea pigo la penalti dhidi yao.
RAIS MALINZI AENDA KUJITAMBUSHA CAF
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameondoka
leo (Februari 17 mwaka huu) kwenye Cairo, Misri kujitambulisha kwa
uongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Akiwa
Cairo, Rais Malinzi ambaye alichaguliwa Oktoba 28 mwaka jana atakutana
na Rais wa CAF, Issa Hayatou pamoja na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo
Hicham El Amrani.
WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA
Wachezaji
watatu wanaocheza mpira wa miguu nchini Tanzania wameombewa Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili wakacheze katika nchi za Thailand na
Ujerumani.
Mchezaji
Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar
es Salaam ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili
akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Said
Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo
wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili
ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara
taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa
Tanzania itatoa ITC hizo.
No comments:
Post a Comment