JESHI la polisi hapa nchini limefanikiwa kuwatia mbaroni vinara wa milipuko ya mabomu hapa nchini, Yusufu Ally (30) na mkewe Sumaina Juma (19), wakazi wa Sombetini, wakiwa na mabomu ya kurusha kwa mkono aina ya Gurnet saba, risasi sita za shotgun, baruti, mapanga mawili na bisibisi moja.
Mtaalamu wa mabomu kutoka Jeshi la Polisi akionyesha kwa waandishi wa habari moja ya bomu lililokamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, alisema kati ya mabomu
hayo moja limetengenezwa nchini Ujerumani na sita yametengenezwa Urusi.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa 2 usiku katika eneo la
Sombetini mjini hapa baada ya jeshi la polisi kupata taarifa juu ya
watuhumiwa hao kuhusika na matukio ya milipuko ya mabomu.
Aliongeza kuwa polisi inamtafuta kinara muhimu wa mabomu, Yahaya
Hussen Hela (35), mkazi wa Mianzini jijini hapa, huku watuhumiwa wengine
25 akiwemo mfanyabiashara maarufu jijini hapa anayemiliki mabasi ya
Kandahal Said Temba (42), pamoja na Imamu wa Msikiti wa Masjidi Qubia,
Japhal Lema (38) ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi wilayani
Arumeru wakishikiliwa kuhusisana matukio ya mabomu.
Miongoni mwa watuhumiwa hao, sita kati yao wanahusishwa na tukio la
ulipuaji wa mgahawa wa Vama uliotokea Julai 7, mwaka huu,na kusababisha
majeruhi wanane raia wenye asili ya Kiasia.
Watuhumiwa
sita wa mlipuko huo wametajwa kuwa ni Shabani Hussen (38)ambaye alikuwa
mlinzi katika mgahawa huo, Mohamed Nuru (30) mlinzi wa mgahawa wa
jirani na tukio, Japhari Lema (38), Abdul Mohamed (31), wakala wa mabasi
stand pamoja na Said Temba (42), wote wakazi wa jijini Arusha.
Mngulu alisisitiza kuwa polisi inaendelea kuwasaka wahuhumiwa wengine
zaidi na kwamba jeshi hilo limeahidi kutoa zawadi kwa atakayeweza kutoa
taarifa za siri zitakazowezesha kupatikana kwa wahusika hao.
Credit: Global publisher.
No comments:
Post a Comment