VITUKO

Wagoni Wapigwa Mawe hadi Kufa Huko Pakistan.

Wagoni

Wagoni Wauawa kwa Mawe.

Wagoni wawili Wanaokadiriwa kuwa na Miaka 30 kila mmoja Wameuwa Kikatili baada ya Kunaswa Wakishiriki Vitendo vya Ngono. Inasadikiwa Kuwa wagoni hao Kila mmoja na Ndoa yake na Kitendo cha Kunaswa Wakivunja Amri ya Sita Imewaghadhabisha Mno Raia wa Baluchistan Magharibi mwa Pakistan.

Aidha waliohusika na Mauaji ya Wagoni hao Wawili wamekamatwa na Polisi kwa Kosa la Mauaji, Baba na Kaka wa Mwanamke Pamoja na Mjomba wa Mwanaume wanashikiliwa na Polisi kwa Kosa Hilo la Mauaji.
Wagoni Wakiuawa kwa Kupigwa Mawe
“Ni kitendo cha Kikatili sana na Watu waliohusika na Mauaji haya ni Lazima Wafikishwe mbele ya Sheria” Alisema Bugti Ambaye ni Balozi wa Eneo Hilo la Magharibi mwa Pakistan

Hali ya Hatari.

Taarifa Zinaeleza Kuwa Kumekuwa na Ongezeko la Matendo ya Kinyama yanayofanyika Nchini Humo Hadi Kufikia Kiasi cha kesi 1000 kila Mwaka huku kukiwa na hofu ya Idadi Hiyo Kuzidi Kuongezeka Zaidi

Hebu Angalia Kituko Alichokivaa Msichana Huyu Katika Ulimwengu wa Fasheni.

Je hii ni sawa, hivi kweli anaweza kukifanya hiki kama kivazi chake rasmi cha mtoko?

Kitu kimoja, kivazi hiki kimenifanya niufikirie huu ulimwengu wa fasheni na hawa wabunifu wetu, hata sielewi ni nini hasa huwa wanakaa na kufikiria kisha kuja na mitindo kama hii...


Mwanafunzi Mwaka wa Kwanza Ajinyonga Baada ya Kufeli Mitihani.

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu  cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.



Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.

Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.

Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao.


AMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA SIGARA.


Uvutaji wa sigara umeleta maafa, baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea sigara.


Katika tukio hilo lililotokea Korogwe, Jumapili iliyopita, Februari 2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa miaka 30 alimkata mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea ugomvi uliohusu sigara.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Massawe alisema kuwa Polisi Tanga wako katika msako mkali wa kumtia nguvuni Iddi Mkono (30) kwa tuhuma za mauaji.

Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.

Wakati huo huo, watu wawili wanashikiliwa na polisi, mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu ya gongo maeneo ya Handeni, mkoani Tanga.

Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.

Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.

Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua tahadhari na matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza kusababisha kuvunja sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria zilizowekwa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. 

No comments:

Post a Comment