Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
KIUNGO
mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anadaiwa
kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake
leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Coastal Union
ya Tanga, Wakundu wa Msimbazi wakifungwa 1-0.
Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.
Polisi walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa.
Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment