Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee
Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Mama
Delfina Mtavilalu mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa
Iringa ambapo alipokelewa na baadhi ya viongozi wa mkoa huo na kuelekea
moja kwa moja ofisini ambapo alifanya mazungumzo mafupi na viongozi hao
na baadae akakutana na waandishi wa habari, Akizungumza na waandishi wa
habari amesema yeye hakkwenda iringa kupiga kampeni kwakuwa kampeni
zinapigwa na kamati za siasa pamoja na viongozi mbalimbali kutokana na
jinzi walivyopangiwa kazi yake yeye ni kuratibu kampeni hizo na kupokea
taarifa za kampeni hizo na kuona kama kamati za siasa za kata zinafanya
kazi, Chama cha Mapinduzi kiko katika kampeni jimbo la Kalenga pamoja na
vyama vingine kikiwa kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa ambapo uchaguzi
wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu.(PICHA NA
KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA)
Akizungumza na waandishi wa habari
huku akionyesha moja ya gazeti lililowahi kuripoti kampeni hizo kwa
picha Philip Mangula amelaani kampeni alizodai zinadhalilisha watoto
zinazofanywa na CHADEMA huku akionyesha mmoja wa watoto ambaye alipigwa
picha huku akionyesha sare zake za shule ambazo zimechakaa na kuchanika
na mmoja wa wapiga debe wa chama hicho akisema kutangaza umasikini wa
mtu ni kumdhalilisha
Philip Mangula akiingia katika ofisi
za mkoa wa Iringa huku akiwa ameongozana na Katibu wa Mkoa wa Iringa Bw.
Hassan Mtenga na viongozi wengine.
Kipande Cha Gazeti hilo kikionyesha picha iliyochapishwa hivi karibuni inayodaiwa kumdhalilisha mtoto.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea zaidi kuhusu picha hiyo
Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Silvanus Kigomba akiuliza swali kwa Mzee Philip Mangula wakati wa mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifafanua zaidi swali la mwandishi huyo
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee
Philip Mangula akielezea mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi huo ambapo
amesema CCM ni waumini wa Amani na kwamba katika jimbo la Kalenga
hagombei Godfrey Mgimwa bali kinachogombea ni Chama cha Mapinduzi kwani
ungekuwa ni ukoo wa mgimwa unagombea basi ungeona akina mgimwa woote
wako mbelea wakipiga debe ili washinde lakini kwa sababu ni CCM
inagombea ndiyo maana utaona viongozi na wana CCM mbalimbali wakishiriki
katika kampeni hizo ili kukipatia ushindi chama chao.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee
Philip Mangula akizungumza nabaadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Iringa
kabla ya kuelekea Ifunda ambako atapiga kambi huko
No comments:
Post a Comment