Na Saleh Ally, Cairo
Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya hapa,
wameamua kuondoka kwenye uwanja ambao wamekuwa wakifanyia mazoezi na
kujichimbia kusikojulikana.
Al Ahly wameamua kufanya hivyo ili
kufanya maandalizi yao kwa utulivu kabla ya kuivaa Yanga katika mechi ya
marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumapili.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar es
Salaam mabingwa hao wa Afrika walilala kwa bao 1-0 lililofungwa na
nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' na kwa mara ya kwanza Yanga
ikafuta uteja wa kufungwa kila inapokutana na Al Ahly.
Lakini mashabiki wao wengine wameeleza
kuwa Ahly wameamua kujichimbia kutokana na vurugu zilizofanywa na
mashabiki wake mara baada ya kupata taarifa kuwa wamefungwa bao 1-0
jijini Dar es Salaam.
"Wakati mwingine imekuwa kawaida Ahl
kuondoka na kujificha sehemu kwa ajili ya maandalizi, lakini safari hii
mambo yamekuwa tofauti kidogo, wanaonyesha wmepania kushinda mechi hii.
"Tokea wamerudi hawajaonekena klabu,
huenda ni hofu ya mashabiki waliokuja kufanya vurugu hapa wakipinga wao
kufungwa na timu kutoka Afrika Mashariki, lakini pia suala la umakini
tu," alisema mmoja wa wafanyakazi kwenye uwanja huo kwa Kingereza cha
tabu.
Championi lilifunga safari hadi kwenye
uwanja huo jana mapema kutaka kushuhudia mazoezi yao, lakini
likaambulia patupu na kuelezwa hivi: "Hutamuona mtu hadi siku ya mechi."
No comments:
Post a Comment