Wanasayansi
nchini Ufaransa wamebaini kwamba virusi vya Ugonjwa wa Ebola ndio
chanzo cha ugonjwa wa homa ya haemorajic nchini Guinea ambayo inaaminika
kuwauwa karibia watu sitini.
Ugonjwa huo ambao unaweza kuambukizwa kwa haraka ulianza nchini humo yapata majuma sita yaliopita.
Dalili za ugonjwa huo ni kutoka damu,kuharisha pamoja na kutapika.
Afisa
mmoja wa wizara ya afya nchini Guinea amesema kuwa takriban visa vinane
vya ugonjwa huo vimeripotiwa hususan kusini mwa taifa hilo.
Amsema kuwa serikali ya taifa hilo inatumia kila njia kukabiliana na ugonjwa huo lakini inaendelea kushindwa.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa Ebola ambao husambazwa kupitia kugusana na walioambukizwa
No comments:
Post a Comment