Watu 100 wamekamatwa mjini Mombasa
Pwani ya Kenya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa ndani ya kanisa moja
mjini humo siku ya Jumapili. Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na
kufunika nyuso zao waliwapiga risasi waumini wa kanisa moja mtaani
Likoni na kuwaua watu wanne Watu walifariki papo hapo wengine
wakifariki hospitalini wakati wakipokea matibabu. Wengine 17
walijeruhiwa vibaya.
Polisi wanasema kuwa watu watatu
waliokuwa wamejihami walivamia kanisa la Joy Jesus na kuanza
kuwafyatulia waumini risasi kiholelea. Kadhalika polisi walisema kuwa
washukiwa wakuu wa shambulizi hilo wametoweka
Hakuna mtu yeyote aliyekiri kufanya
mashambulizi hayo , ila Kenya imekuwa ikishuhudia ongezeko la
mashambulizi tangu kuanza kujihusisha na vita nchini Somalia mwaka 2011.
Jeshi la Kenya linasaidiana na wanajeshi wa Muungano wa Afrika
kupambana na kundi la wanamgambo la Al Shabaab.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini
humo kufuatia shambulizi hilo ambalo limekuja siku chache tu baada ya
polisi kunasa washukiwa watatu wa ugaidi wakiwa na mabomu mawili makubwa
tayari kufanya shambulizi kubwa. Pia walinasa vilipuzi vingine ndani ya
gari lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi. Mji wa Mombasa
wenye sifa ya utalii, umekuwa ukikumbwa na suitofahamu ya kiusalama
kutokana na vijana wengi kujiunga na itikadi kali za dini hiyo.
No comments:
Post a Comment