MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,
jijini Dar es Salaam, imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi Mawaziri
Waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wanaokabiliwa na
tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara
ya Sh. bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi baada ya kusikiliza
maombi yao leo.
Uamuzi
huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya
washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Jaji
Utamwa alisema baada ya kusikiliza maombi hayo mahakama inawaruhusu
washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na
ruhusa hiyo Mramba na Yona siku ya kusikiliza kesi Aprili 22, mwaka huu
wahudhurie mahakamani.
Mbali na Mramba na Yona, mshtakiwa mwingine ni, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.
Katika
kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na
Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama
mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa
kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza
iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu
ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia
mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha
Sheria ya Manunuzi ya Umma.
No comments:
Post a Comment