Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akionesha
mbele ya waandishi wa habari Ofisi kwake meno ya tembo vipande 2 yenye
thamani ya shilingi 22 hapo jana aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Batromeo
Mtongwa hapo machi 8 katika kijiji cha kilida katika tarafa ya mamba
wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na gobole 1 na
risasi 14.
Mkazi wa kijiji cha kilida tarafa ya mamba wilaya ya mlele, Patromeo
Mtongwa (58) akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi baada ya
kukamatwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani
ya shilingi milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14 mtuhumiwa
alikamatwa hapo machi 7 mwaka huu majira ya saa mbili usiku nyumbani
kwake katika kijiji cha kilida.
Na Walter
Mguluchuma Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Bathromeo James
Mtongwa 58Mkazi wa Kijiji cha Kilinda Tarafa ya Mamba
Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi amekamatwa akiwa nameno vipande
viwili vyenye uzito wa kilo 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja
na Bunduki moja aina ya Gobore na Risasi 14
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi msaidizi mtuhumiwa
huyo alikamatwa hapo machi
7 mwaka huu majira ya saa mbili
na nusu usiku
Alisema mtuhumiwa
alikamatwa kufutia taarifa ambazo ambazo zililifikia jeshi la polisi
pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kupata taarifa kuwa
mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume
cha sheria ambapo taarifa hizo zilipatikana hapo
machi 6 kutoka kwa Raia wema
Alifafanua ndipo
siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na Askari wa Hifadhi
ya Taifa ya Katavi walifika
kwenye kijiji hicho cha
Kilinda nyumbani kwa mtuhumiwa Batromeo
na kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanikiwa
kukamata risasi 14
Kidavashari
alieleza wakati askari hao wakiendelea
na upekuzi kwa kushirikiana na uongozi
wa kijiji walilitilia shaka eneo moja la nyumba hiyo ya mtuhumiwa
kutokana na eneo hilo
kuonekana kuwa limechimbwa
Alisema ndipo
askari walipoamua kuchimba eneo hilo na
baada ya kufukua kwa kitambo kidogo
walifanikiwa kukuta meno ya Tembo
vipande viwili vyenye uzito wa kili 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22
yakiwa yamefukiwa ardhini kwenye shimo
Baada ya
kukamatwa kwa maneno hayo ya Tembo polisi walianza kumhoji mshitakiwa kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa
akiifadhi Silaha ambayo amekuwa
akiitumia kwenye matukio ya ujangili
Kidavashari alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa aliweza kueleza kuwa bunduki ambayo amekuwa
akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameifisha
kwenye eneo linaloitwa King’anda
lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Alisema siku
ya tarehe 8 machi majira ya saa nane
mchana mtuhumiwa aliwaongoza
Askari Polisi na Askari wa
Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuwapeleka
katika eneo la King’anda ndani ya
Hifadhi ya Katavi na aliweza kuwaonyesha silaha hiyo Bunduki aina ya Gobore ikiwa imeifadhiwa kwenye kichaka
Mtuhumiwa anatarajiwa
kufikishwa Mahakamani wakati wawote
mara baada ya upelelezi wa tukio
hili utakapo kuwa umekamilika mapema
iwezekanavyo pia jeshi la polisi Mkoa wa
Katavi lanatowa wito kwa wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi kwa kutowa taarifa za watu
wanaojihusisha na uwindaji haramu wa rasilimali za Taifa ili kulinda na kuhifadhi
rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo
No comments:
Post a Comment