Nyota wa kimataifa kwenye soka ambaye ni mchezaji mwenye umri wa miaka 53 kutoka Argentina Diego Maradona amekuwa katika mazungumzo na klabu
ya Deportivo Riestra, ambayo inashiriki ligi ya chini kabisa kwa lengo la kujiunga nao kama mchezaji mpaka kumalizika kwa msimu.
Nchini
kwake ni maarufu kwa jina ‘God’ Maradona amekuwa akipambana na uzito
katika siku za hivi karibuni kwa lengo kujiweka sawa na fiti kabla ya
kuanza mchezo wake wa kwanza March 23.
Mmoja
wa wachezaji wa Deportivo Kiungo Victor More, amesema yuko tayari kuvua
jezi yake nambari 10 anayovaa sasa na kumkabidhi Maradona atakapo saini
kuichezea klabu hiyo na pengine mkongwe huyo anayetumia mguu wa kushoto
akarejea kuitendea haki jezi hiyo aliyokuwa akiivaa enzi zake.
No comments:
Post a Comment