Ilikuwa Wiki ya Majonzi kwa mashabiki
wa soka nchini Tanzania baada ya wawakilishi wao kwenye Michuano ya Soka
kuwania Kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC kutupwa nje ya
michuano hiyo kufuatia Kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Feroviario de Beira
ya Msumbiji hapo jana Jumapili mjini Beira.
Kufuatia kichapo hicho cha ugenini
Azam imeaga michuano hiyo kwa kichapo cha bao 2-1 kufuatia ushindi
mwembamba wa bao 1-0 iliokuwa imeupata katika mechi ya awali mjini Dar
es Salaam.
Kwa matokeo hayo Azam imeaga michuano
hiyo na kuiacha Yanga ya Dar es Salaam kubeba bendera ya matumaini ya
Watanzania kwenye Michuano ya kuwania Klabu Bingwa barani Afrika ambapo
sasa inajiandaa kuikabili National Al Ahly ya Misri ambao ni Mabingwa
watetezi baadae mwezi huu,baada ya kuitupa nje Comorozine ya Comoro kwa
ushindi wa jumla wa bao 12-2.
Mechi hiyo ya Yanga dhidi ya Mabingwa
hao wa Afrika Al Ahly ,tayari imeshaanza kuwa gumzo kubwa jijini Dar es
Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla hasa kutokana na historia uimara wa
Timu za Misri hususan kwenye Michuano ya soka barani Afrika,ambapo kwa
miaka Mingi Timu kutoka Misri zimekuwa zikizitesa klabu za Tanzanzia
hususan Simba na Yanga ingawa Timu ya Simba mwaka 2003 ilifanikiwa
kuivua Ubingwa Zamalek na kuweza kutinga hatua ya nane bora katika
kuwania Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika
Chanzo, bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment