Monday, February 17, 2014

“NI MARUFUKU KUTUMIA PESA KUNUNUA MADARAKA YA UONGOZI”….MEMBE

membe
WAZIRI  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe
,amesema kuwa ni mwiko kwa mtu yeyote ndani ya chama kutumia fedha
kama nguzo ya ushindi wake kwa kuwa uongozi wa taifa hauwezi
kununuliwa na fedha.
Membe ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(NEC) Mbali na hilo pia amekitaka chama hicho kufika mahala kuchagua ni nani anayefaa kuwa kiongozi kwa kufanya midahalo ili kutambulika kwa wananchi na kuepuka chama kumegukameguka.
membe
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kutoka kuhojiwa na kamati ndogo ya maadili ya chama
hicho ambayo ilikaa tangu alhamis ya wiki iliyopita kwaajili ya
kuwahoji makada sita ambao wamejitangaza kuwania urais katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 kinyume na sheria na taratibu.
Membe alitinga katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM majira ya saa
tatu asubuhi na kutoka saa 4:54 asubuhi.
Alisema kuwa haiwezekani kuwa na kiongozi anayenunua uongozi kwa njia
yeyote ile, iwe ya fedha au jambo lolote na hilo ndilo kamati ya
maadili inakemea na yeye anaungana nayo.
“Lakini waandishi habari lazima wawe objective, waandishi lazima
mmpime, , waandishi wa habari ndio mnaoweza kuamua direction iende
wapi, lazima muandike ya watu wote wanayozungumza bila kuchagua mambo
Fulani ya mtu Fulani,”.
“Nawaambia waandishi chezeni mtaona, hatuwezi kuruhusu uongozi wa nchi
hii  au kiongozi wa juu anunuliwe kama biashara ya njugu dukani,
tukiacha hilo liendelee ninyi waandishi wa habari ni sehemu ya watu wa
kulaumiwa duniani,”alisema Membe
Alisema taifa la Tanzania litakuwa ni la ajabu kama watanzania
wataruhusu kufanya kufanya biashara ya uongozi wa kitaifa.
Hata hivyo alisema kuwa ni vyema sasa chama kikajipanga kuwa na
Mgombea ambaye wanachama wajue ni nani atakayepeperusha Bendera katika
uchaguzi wa Mwakani.
“Kwa mfano ili wananchi wajue tupokwenda mwaka 2015 candidate wa chama
ni nani, lazima tufike hapo tukiacha kila mwanachama aombe kila
binadamu anayeona anaavaa nguo ya kijani au ana hela aombe,
tutakiangusha chama chetu…Nadhani tunashauri chama kikajipange na
kiwe na candidates yaani kiwe na watu ambao  inabidi harakahara
wapitishwe ili CCM kinapofika desemba kwa mfano tuwe tunajua nani
anachukua bendera ya chama ili kisimegukemeguke,”alisema Membe
Aidha alisema kuwa alishauri kuwepo na muongozo rasmi unaotakiwa
kufuatwa na wanaccm kuanzia katika ngazi za matawi mpaka juu.
“Wakati wa uongozi utumie hatua zipo ili uzingatie nini ili usivunje
maadili, mashabiki nao wafanye nini ili wasikiuke maadili ili tuweze
kwenda pamoja kwa hiyo ni kamati ya maadili inayouliza maswali magumu
sana kwa watu wanaosemwa kwamba  wanaweza kuwa viongozi,”alisema Membe
Alisema kuwa kamati ya maadili inataka chama hicho mwakani kiende
katika uchaguzi kiwe imara na kuungana ili kuhakika wa ushindi na CCM
iendelee kupeta miaka 60 ijayo hakuna atakayeingia.
“Mimi ni miongoni mwa watu tulioitwa na kamati ya maadili, kamati
imefanya kazi nzuri, imedhamilia kumuita kila mtu anayetajwa kuwa
anaweza kuwa kiongozi,”alisema Waziri huyo.
Hata hivyo alisema kuwa kamati ya maadili imejipanga vizuru sana na
wasidanganyike.
“Wanauliza maswali magumu ama unayoyafanya wewe au wanayoyafanya
mashabiki lakini yote yanalenga chama chetu, kuimarisha ushindi 2015
na katika kuimarisha maadili,”alisema Waziri huyo
Hata hivyo alisema kuwa kumekuwepo na uzukaji ghafla wa
makundi makubwa ambayo yamezaliwa na kila watu wanadhani fulani
anafaa kuwa kiongozi.
“Tutafaanyaje nini ili chama kiwe na kundi moja litakalokwenda mwakani
kwenye ushindi na suala la fedha kama msingi wa ushindi, inatokeaje
watu wanatumia mamilioni mabilioni ya pesa katika kujinufaisha na
kujiandaa
kwenda kwenye uchaguzi,”aliema Membe
Aliitaka kamati ya maadili iendelee kuifanya  kazi hiyo na kudai kuwa
bado kuna wengine wataitwa lengo ni kuwa na chama imara ambacho
kitakwenda kwenye uchaguzi mwakani kwenda kuvishinda vyama vingine
vinavyojitokeza na vingine ambavyo vimeshaanza kufa.

No comments:

Post a Comment