Wednesday, February 26, 2014

DAKTARI FEKI AKAMATWA TENA MUHIMBILI AKITAPELI WAGONJWA


Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali

Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.

Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza.

Hospitali ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.

Chama cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa  macho na madaktari wanaojitokeza kutaka kusaidia wagonjwa.

Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni feki.

Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment