Habari za hivi punde zinasema kuwa
Mamia ya polisi wanakabiliana na waandamanaji ambao wamekita kambi
katika afisi za serikali kuanzia mwezi desemba kwa niya ya kuwangoa.
polisi wakimtia nguvuni mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa watu wanaofanya vurugu katika eneo hilo
Mkuu wa polisi Major-General Adul
Dam-rong-sak anasisitiza kuwa ni lazima waandamanaji hao waruhusu
uchukuzi na hali ya kawaida kurejea katika jiji hilo Bangkok
Duru zimeiambia BBC kuwa takriban
Waandamanaji 100 wamekamatwa katika operesheni hii ya kwanza tangu mwezi
Desemba waandamanaji hao walipovamia afisi za umma mjini Bangkok
wakipinga utawala wa Waziri mkuu Yingluck Shinawatra.
Waandamanaji wanadai kuwa Yingluck ni kikaragosi cha kakake aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja Thaksin Shinawatra ambaye yuko uhamishoni.
Waandamanaji wanadai kuwa Yingluck ni kikaragosi cha kakake aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja Thaksin Shinawatra ambaye yuko uhamishoni.
Wengi wanaompinga Yingluck wanataka
aondoke malakani na badala yake kuchaguliwe baraza la watawala
litakaloongoza Thailand hadi uchaguzi ufanyike.
Kiongozi wa upinzani, Suthep Thaugsuban aliwaambia waandamanaji kuwa anapigania utawala na madaraka ya Wathai kurudishia umma .
"hatupigani na serikali ilitujiweke
madarakani sisi wenyewe bali tunataka vizazi vijavyo vijitawale
"Uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ulisusiwa na makundi ya upinzani
kwa sababu ilitarajiwa kuwa waziri Yingluck na chama chake wangeibuka
washindi.
Yingluck alichaguliwa mnamo mwak wa 2011 kutokana na ufuasi mkubwa kutoka maeneo ya mashambani ya Thailand.
Chanzo, bbcswahili
No comments:
Post a Comment