Rufiji. Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Seif Rashid amesema mwishoni mwa mwezi huu Serikali itatumia
Sh4 bilioni kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 14 vilivyopo
kwenye Kata ya Ikwiriri na Mloka mkoani Pwani.
Akizungumza jana wakati alipokutana na
wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) wa Wilaya ya Rufiji
walipokuwa kwenye sherehe ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribish mwaka huu,
Dk Rashid alisema mradi huo utatekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijijini(REA) ambapo watasambaza katika vijiji hivyo mwishoni mwa mwezi
huu .
Alisema katika utekelezaji wa mradi
huo, huduma za kijamii zitapewa kipaumbele katika kuunganishiwa nishati
hiyo ikiwamo shule, zahanati, Visima vya maji, misikiti na makanisa na
kwamba mradi huo wa umeme utainua kiwango cha ubora wa maisha ya
wananchi. chanzo MWANANCHI
No comments:
Post a Comment