Makongoro Nyerere
MSHITAKIWA Makongoro Nyerere anayekabiliwa na kesi ya mauaji ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imuachie huru akaishi na watoto wake au ajiue.
Makongoro alidai hayo jana mbele ya
Hakimu Mkazi Hellen Liwa, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali,
Inspekta Jackson Chidunda kudai upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika.
Makongoro, ambaye ameshitakiwa pamoja na
mfanyabiashara maarufu Abubakar Marijan (50), ‘Papaa Msoffe’ aliomba
mahakama imuachie huru kwa kuwa hana kesi, alikuwa anafanya kazi halali
lakini ameambiwa ameua, kisa Sh milioni nane.
Makongoro Afunguka
“Tarehe nyingine kesi itakapotajwa naomba niachiwe nikakae na watoto wangu niende nikakae polisi, huko watajua pa kunipeleka kama kujiua nijiue,” aliomba Makongoro.
Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi
Machi 11, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Aliutaka upande wa
Jamhuri kuharakisha upelelezi. Jana Papaa Msoffe hakufika mahakamani
hapo kwa madai kuwa anaumwa.
Washitakiwa wanadaiwa Oktoba 11, mwaka
2011 katika eneo la Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam kwa makusudi
walimuua Onesphory Kituli.
Hawakujibu mashitaka kwa kuwa mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na
wataendelea kusota rumande kwa kuwa mashitaka yao hayana dhamana.
No comments:
Post a Comment