Wanafunzi waliodaiwa kunusurika kusafirishwa hawa hapa
……………………………………………………………………
HUKU
mkoa wa Iringa ukiwa katika vita vikali vya kuwalinda watoto wa
kike kutoka mkoani hapa kwenda mijini kufanyishwa kazi za ndani (uyaya)
na katika madangulo ,watoto wa kike wameendelea kugeuka dili kubwa
mkoani Iringa baada ya mwamake mwingine mjini hapa kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma za kusafirisha watoto wa kike sita kwenda
kuuzwa kwa ajili ya kufanya kazi za ndani mijini
Kukamatwa
na kufikishwa mahakamani kwa mwanamke huyo kunaendelea kutishia
usalama wa watoto wa kike katika mkoa wa Iringa kutokana na wimbi
hilo la usafirishaji watoto wa kike kwenda mijini baada ya mwezi huu
mmoja kukamatwa wanawake wawili kwa kujihusisha na biashara hiyo ya
watu.
Mwanamke
wa kwanza alikamatwa eneo la Frelimo akitaka kumtorosha mfanyakazi wa
ndani na kuishia kupewa kichapo kama adhabu yake ya kufanya
biashara hiyo ya watu .
Wakati
tukio jingine ambalo linafanana na hilo limetokea mwanzoni mwa wiki
hii baada ya mwanamke mmoja Bi Amina Sanga (42) ambae ni mke wa
aliyepata kuwa mfanyabiashara maarufu mjini hapa kujikuta akifikishwa
mahakamani kwa tuhuma za kutaka kuwasafirisha watoto sita wa kike
kwa ajili ya kwenda kufanyakazi za ndani mijini.
Mwanamke
huyo ambae alifikishwa siku ya jumanne wiki hii mbele ya hakimu wa
mahakama ya mwanzo Bomani mheshimiwa Alois Masua alipata kusomewa
shitaka hilo la jinai namba 33 la mwaka huu .
Akisoma
shitaka hilo hakimu Masua alisema kuwa mwanamke huyo mkazi wa Mgela
Iringa vijijini anatuhumiwa kwa kosa la kusafirisha watoto sita wa
kike ambao ni wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya
Sekondari Mgela.
Kuwa
mshitakiwa huyo alikamatwa majira ya saa 10 alfajiri ya mwishoni mwa
wiki kutokana na mtego uliowekwa na wananchi wa eneo hilo.
Katika
kesi hiyo mlalamikaji ni mtoto Sophia Kitule kwa niaba ya wenzake
watano ,mshitakiwa alikana shitaka hilo na mahakama hiyo kudai kuwa
dhamana yake ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja akiwa na barua
ya dhamana ya Tsh milioni 1 na mali isiyohamishika .
Hata
hivyo mshitakiwa huyo alilazimika kwenda mahabusu hadi tarehe 12 ya
mwezi ujao baada ya wadhamini wao kukosa sifu baada ya kufika
mahakamani hapo wakiwa mikono mitupu bila barua .
No comments:
Post a Comment