Sunday, February 23, 2014

BAADA YA KULALAMIKA, SASA POSHO YA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUWA SH. 500,000/=



Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku.

Habari zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la jana kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli.


Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi.


Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura.

No comments:

Post a Comment