Jana mida ya Jioni pale mlimani City
nimeshuhudia wafanya kazi wa Duka Kubwa la Shoprite wakiwa wamegoma
wakizua watu wasiingie kwenye duka hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa duka
hilo limeuzwa bila wao kupewa mafao yao …Habari zilizopo ni kuwa duka
hilo limenunuliwa na Super Market Ingine kubwa Nchini Kenya Ambayo
inakuja kupanua biashara zake hapa Dar …..
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni
mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi
Bilioni 480 kwa mwaka. Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Mawsiliano
wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana
na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la
Engaruka Wilayani Monduli mkoani Arusha. Alizitaja faida za kugundulika
kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni
kutokana na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.
Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea
magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa
sekta ya viwanda hapa nchini. Ngapemba alibainisha kuwa madini ya magadi
soda yanatumika viwandani katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo,
sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza
karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.
Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na
wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu
tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya
kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda. Alisema
kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni
kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC
Service.
"Matokeo ya utafiti huo yameonyesha
kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na
inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka
katika eneo hilo," alisema Ngapemba na kuongeza: Alisema kuwa NDC
itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira
hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika
hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
CHANZO:The Habari.com