Thursday, February 20, 2014

Wakenya Walalamikia Katiba Mpya Kuwalazimisha kulipa Ushuru wa Kuaga Maiti na Kuchinja Mifugo yao.


funeral
Kenya ilizindua Katiba mpya Agosti 27 mwaka 2010 kwenye sherehe iliyojaa mbwembwe katika bustani ya Uhuru,hatimaye katiba hiyo imeanza kuwapa machungu ya kulazimika kulipa ushuru wa kuaga maiti pamoja na kulipa ushuru wakuchinja mifugo yao.
Inatafsiriwa kuwa, magavana wametumia mamlaka yao kunyanyasa wananchi katika kaunti. Katika Kaunti ya Kiambu, inayoongozwa na Gavana William Kabogo, kuna ushuru mpya unaotozwa kwa familia iliyopoteza mpendwa ama wapendwa wao. Hakuna anayekubaliwa kumzika mfu wao bila kulipa ushuru huo. Pia, huwezi kuchinja mfugo wako nyumbani bila kulipa ushuru!
Katika Kaunti ya Kakamega, Gavana amebuni ushuru wa kuku ambapo kila mfugaji atalipa Sh20 kwa kila kuku anayemfuga.
Pia, watu wanapoomboleza, lazima walipe ushuru wa kuomboleza haswa wanapotazama mwili wa marehemu.
Ukiutazama zaidi ya mara mbili, utalipa ushuru zaidi ya mara moja!
Watu hawajui la kufanya na wana majuto makuu kwa kukaribisha Katiba mpya 2010. Walipokuwa wanaipitisha walikuwa na matumaini kwamba ingebadilisha maisha yao kwa kuleta utawala na huduma za Serikali Kuu karibu yao.
Wakati huo wa mchakato wa Katiba mpya, Makamu wa Rais William Ruto alikuwa katika upande uliokuwa ukipinga Katiba hiyo.
Source:Mwananchi

No comments:

Post a Comment