Monday, February 17, 2014

BIASHARA YA KUSAFIRISHA MABINTI YAIBUKA IRINGA

mabinti
 Wanafunzi  waliodaiwa  kunusurika  kusafirishwa  hawa  hapa 
……………………………………………………………………
HUKU mkoa wa Iringa  ukiwa katika  vita  vikali  vya  kuwalinda  watoto  wa kike kutoka mkoani hapa kwenda mijini kufanyishwa kazi za ndani (uyaya) na katika madangulo ,watoto  wa kike wameendelea  kugeuka dili kubwa mkoani Iringa baada ya mwamake  mwingine mjini hapa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusafirisha  watoto wa kike  sita  kwenda  kuuzwa kwa ajili ya kufanya kazi za ndani mijini 
  
Kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mwanamke  huyo kunaendelea kutishia usalama  wa watoto wa kike katika mkoa  wa Iringa  kutokana na wimbi hilo la usafirishaji  watoto wa kike kwenda mijini baada ya mwezi  huu mmoja kukamatwa  wanawake wawili kwa kujihusisha  na biashara  hiyo ya  watu.

Mwanamke  wa kwanza alikamatwa eneo la Frelimo akitaka kumtorosha  mfanyakazi wa ndani na kuishia kupewa kichapo kama adhabu  yake  ya  kufanya  biashara  hiyo ya  watu .

Wakati  tukio jingine ambalo linafanana na  hilo limetokea  mwanzoni mwa wiki  hii baada ya  mwanamke  mmoja  Bi Amina  Sanga (42) ambae ni mke wa aliyepata  kuwa mfanyabiashara  maarufu mjini hapa kujikuta  akifikishwa mahakamani kwa  tuhuma za  kutaka  kuwasafirisha  watoto sita  wa kike kwa ajili ya kwenda  kufanyakazi za ndani mijini.

Mwanamke  huyo ambae  alifikishwa  siku ya jumanne  wiki  hii mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo Bomani mheshimiwa Alois Masua alipata  kusomewa  shitaka   hilo la jinai  namba 33 la mwaka huu .

 mabinti
Akisoma  shitaka  hilo hakimu Masua  alisema kuwa mwanamke  huyo mkazi wa Mgela  Iringa vijijini  anatuhumiwa  kwa kosa la kusafirisha  watoto  sita  wa kike ambao ni wanafunzi wa  kidato cha kwanza katika shule  ya Sekondari Mgela.

Kuwa mshitakiwa  huyo alikamatwa majira ya saa 10 alfajiri ya mwishoni mwa wiki  kutokana na mtego uliowekwa  na  wananchi wa eneo hilo.

Katika  kesi  hiyo mlalamikaji ni mtoto  Sophia Kitule kwa niaba ya  wenzake  watano ,mshitakiwa alikana shitaka  hilo na mahakama  hiyo kudai  kuwa dhamana yake ya kuwa na  wadhamini  wawili  kila mmoja akiwa na barua ya  dhamana ya Tsh milioni 1 na mali  isiyohamishika .

 Hata  hivyo mshitakiwa  huyo alilazimika  kwenda mahabusu  hadi tarehe 12 ya mwezi  ujao  baada ya  wadhamini  wao  kukosa  sifu baada ya  kufika mahakamani hapo wakiwa mikono mitupu bila barua .

No comments:

Post a Comment