Timu ya Real Madrid ndio mabingwa wa mwaka huu wa kombe la Copa del Rey .
Madrid waliwacharaza wapinzani wao wa
jadi katika ligi ya nyumbani La liga Barcelona mabao 2 kwa 1 katika
fainali iliyochezwa jana mbele ya mfalme wa Uhispania .
Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti
alikuwa anajikuna kichwa kwani mshambulizi wake nyota Cristiano Ronaldo
hakuwa uwanjani kutokana na jeraha la mguu na hivyo ikambidi kumchezesha
mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa
zaidi msimu huu Gareth Bale .
Na alidhibitisha udedea wake alipofuma
bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tano tu mechi hiyo kukamilika na
hivyo kuisadia kutwaa taji lake la 19 la Kombe hilo la mfalme la Copa
del rey.
Real Madrid ilidhibitisha niya yao mapema kwa bao la dakika ya 11 Angel Di Maria
Lakini ikasawazishwa na bao la Bartra katikadakika ya 68 ya kipindi cha pili.
Bao la ushindi lilifungwa na Gareth Bale dakika tano tu kabla ya mechi hiyo kukamilika .
Bale alitimuka mbio na kumpiku mlinzi
wa Barca Marc Bartra katikati ya kiwanja na akafululiza hadi akampiga
chenga kipa machachari Jose Manuel Pinto na kuihakikishia Madrid
ushindi.
Real Madrid bado iko mbioni kuwania
kombe la ligi ya Uhispania, ambapo inashikilia nafasi ya pili na alama
79 alama tatu nyuma ya wakinzani wao Athletico Madrid.
Barcelona ambayo imekuwa ikishuhudia
msururu wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika siku za hivi punde
inafunga orodha ya tatu bora ikiwa na alama 78.
Madrid sasa inamuda wa kutoka
kujiandaa kwa mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya
dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich ya Ujerumani.
Mechi nyingine ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya itakuwa kati ya Chelsea ya Uingereza dhidi ya Atletico Madrid.
Nusu fainali hizo zitachezwa juma lijalo.
No comments:
Post a Comment