Katibu Mkuu
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke
anawasili nchini Leo (Mei 1 mwaka huu) ambapo atafungua semina ya
mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Valcke ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye leo hiyo hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment