Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba
Na Michael Ngilangwa
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba amelejea tena kusisitiza kauli
ya serikali ya kuwataka wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni
pamoja na kuwakamilishia mahitaji mbalimbali ya shule ili kuwepo kwa
mahudhurio mazuri ya wanafunzi na kuboresha kiwango cha taaluma.
Akizungumza
na mtandao huu Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba ameziagiza
kamati na bodi za shule mbalimbali zilizopo katika halmashauri Ya
Wilaya ya Njombe kuhakikisha zinasimamia ujenzi wa miundombinu ya vyoo
huku wazazi wakitakiwa kuwanunulia mahitaji ya shule na kuwaweka watoto
katika mazingira ya usafi.
Aidha bi.Dumba amesema kuwa katika
ziara zake za kutembelea maeneo mbalimbali wilayani Njombe kukagua
utekelezaji wa miradi amebaini kuwepo kwa tatizo la baadhi ya shule
kukosa huduma za chakula,wanafunzi kutokuwa na sale za shule pamoja na
kukosekana kwa vyoo bora kwa maeneo yote ya shuleni na nyumbani.
Amesema
kuwa kukosekana kwa huduma bora za vyoo zinaweza kusababisha mripuko wa
magonjwa katika maeneo ya shule na nyumbani ambapo amewataka wataalamu
wa afya wa kata na vijiji kutembelea maeneo hayo ili kukagua na
kuhimiza usafi wa mazingira katika maeneo ya shule na makazi ya
wananchi na kujikinga na mlipuko wa magonjwa hayo Huku kamati na bodi
akizitaka kupeleka miundombinu ya maji kwa kushirikiana na wananchi ili
vyoo viweze kutumia maji.
Katika hatua nyingine Bi.Dumba
amewataka wananchi kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na
kwamba hatua kali zinatakiwa kuchukuliwa kwa baadhi wanaoendekeza tabia
hiyo ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa watoto huku akiwataka viongozi wa
serikali za vijiji na kata kudhibiti tabia hiyo isiendelee kwani ni
kitendo cha kumkandamiza mwanamke na mtoto.
No comments:
Post a Comment