Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi
kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Perseko Kone kufuatia vifo vya watu 19
wakiwemo askari Polisi wanne na viongozi watatu wa Kijiji katika
ajali ya barabarani iliyosababishwa na basi la Sumry lililokuwa
likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam katika barabara kuu ya
Singida- Dodoma.
Aajili hiyo ilitokea usiku wa tarehe 27
Aprili, katika Kijiji cha Utaho Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida baada
ya basi la Kampuni ya Sumry lenye nambari ya T799 BTE aina ya Nissan
kuwagonga watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo ambalo ajali
nyingine ilikuwa imetokea wakiwaamo na askari Polisi kutoa msaada
katika ajali nyingine iliyokuwa imetokea katika eneo hilo ambayo
mwendesha baiskeli aligongwa na lori na kufariki papo hapo.
Rais Kikwete amesema amepokea kwa
masikitiko vifo vya watu hao 19 wakiwemo askari polisi wanne na
kuongeza kuwa kama taifa vifo hivyo vimelipotezea taifa nguvu kazi
muhimu kwa unjenzi wa taifa na kuacha simanzi na huzuni kubwa familia
ndugu jamaa na marafiki wa marehemu.
Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Perseko Kone kumfikishia salamu zake za rambirambi na pole
nyingi kwa watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kutokana na
ajali hiyo, na amewahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao katika
kuomboleza msiba huo mkubwa.
No comments:
Post a Comment