"
Mtoto wa Mfalme wetu ni mgonjwa kitandani. Mikoba ya waganga wetu wote
bora imemiminia dawa zote zilizokuwamo ndani yake. Haikutokea hata dawa
moja kuwa mujarabu. Hatari ya maisha ya mtoto inahofiwa sana. Mfalme
astahili msaada wa kila raia. Wanatakiwa watu wawili; mwerevu na mjinga,
kwa kafara. Idhini ya Baraza hili yatafutwa. Heshima kubwa kama hii
bado kutokea. Idhini ikipatikana kafara litafanywa mara moja.
Inatazamiwa kuwa salama ya mtoto wa Mfalme imetegemea Baraza hii.
Tumepewa fahari ambayo nchi yo yote ulimwenguni bado kuwapa washauri
wake."- Shaaban Robert
No comments:
Post a Comment