Wanasayansi nchini
Marekani wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi
maisha marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia
viwandani.
Watafiti walichunguza zaidi ya watu
elfu nne waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana
uwezekano mkubwa wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .
Vyakula ambayo havijapitia viwandani
vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika
kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment