Na Magreth Kinabo, Maelezo
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene amesema Jaji Joseph
Warioba alitunukiwa tuzo ya muungano iliyotukuka kwa kuwa alistahili kupewa kama viongozi wengine na kuwa kitendo si kumkejeli kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hivi karibuni.
Hayo
yalisemwa leo na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu suala hilo katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika kwenye Ukumbi wa MAELEZO jijini Dares Salaam.
“Kumekuwa
kuna taarifa katika baadhi ya magazeti kuwa Serikali kumpa tuzo Jaji
Warioba ni kumkejeli, Ninapenda kuwataarifu kuwa kitendo cha Serikali
kumpa tuzo Jaji Warioba haikumkejeli wala kumtukana. Jaji Warioba
anastahili kupewa tuzo kama mawaziri wakuu wengine kwa kuwa mchango wake
katika muungano unajulikana,” alisema Mwambene.
Tuzo hiyo aliyoipewa Jaji Warioba, wakati wa maadhimisho ya mika 50 ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar.
Mwambene aliongeza kuwa tuzo hiyo haihusiani na mjadala wa Rasimu ya Katiba. Alifafanua
kuwa katika mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Katiba
uliokuwa ukifanyika katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, baadhi
ya wajumbe walikuwa wanatoa mawazo yao na si kwamba wanapingana na Jaji
Warioba.
“
Mjumbe anatoa mawazo yake wakati wa kujadili kwa kuwa hiyo bado ni
rasimu, hivyo hapingani na Jaji Warioba,” alisisitiza huku akisema
rasimu huwa inafanyiwa marekebisho.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi huyo , alisema bado Ofisi yake inaendelea na
hatua ya pili kuhusu gazeti la MAWIO kutoa maelezo ya kuchapisha habari
yenye kichwa cha habari ‘Hati Muungano Utata’.
Mwambene
alifafanua kuwa ofisi hiyo inaendelea na suala hilo kwa hatua hiyo ili
kutoa nafasi kwa viongozi husika wa gazeti kutoa maelezo baada ya hapo
awali kupeleka barua ya kutaka maelezo hayo kwenye Ofisi za gazeti la
‘MAWIO’ na kukuta zimefungwa.
Aidha
alisema kuwa hata majirani wa ofisi hizo walikataa kupokea barua hiyo,
kwa maelezo kuwa kama ni masuala ya habari wahusika ndio wanapaswa
kuipokea.
Aliongeza kwamba ofisi yake itafanya maamuzi sahihi ikiwahaitapata maelezo hayo, hivyo isijeikalaumiwa.
Mwambene
aliwataka waandishi wa habari kuwa na kitambulisho cha uandishi wa
habari (Press Card) na ametoa muda wa wiki moja kuanzia leo kwa
mwandishi ambaye hana ili kuweza kukamilisha taratibu za kukipata.
Pia
amewataka waandishi wa habari kuwa na heshima katika utendaji kazi wa
taaluma hiyo na kuzingatia mavazi yanayostahili kwani wao ni kioo cha
jamii.