Wednesday, April 30, 2014

KATIBU MKUU WA FIFA KUWASILI NCHINI LEO

SERIKALI NA WAASI WA SUDAN KUSINI WADAIWA KUWATUMIA WATOTO VITANI

RAIS JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA SINGIDA KUFUATIA AJALI ILIYOUA WATU 19

IGP, DCI WALA KIAPO CHA KUWA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA




DC NJOMBE AWATAKA WAZAZI KUWASILISHA CHAKULA KWA AJILI YA WANAFUNZI SHULENI


 
Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba
 
Na Michael Ngilangwa
 
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba amelejea tena kusisitiza kauli ya serikali ya kuwataka wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni pamoja na kuwakamilishia mahitaji mbalimbali ya shule  ili kuwepo kwa mahudhurio mazuri ya wanafunzi na kuboresha kiwango cha taaluma.


Akizungumza na mtandao huu Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba ameziagiza kamati na bodi za shule mbalimbali zilizopo katika halmashauri  Ya Wilaya ya Njombe kuhakikisha zinasimamia ujenzi wa miundombinu  ya vyoo huku wazazi wakitakiwa kuwanunulia  mahitaji ya shule na kuwaweka watoto katika mazingira ya usafi.


Aidha bi.Dumba amesema kuwa katika ziara zake za kutembelea maeneo mbalimbali wilayani Njombe kukagua utekelezaji wa miradi  amebaini kuwepo kwa tatizo la baadhi ya shule kukosa huduma za chakula,wanafunzi kutokuwa na sale za shule pamoja na kukosekana kwa vyoo bora kwa maeneo yote ya shuleni na nyumbani.


Amesema kuwa kukosekana kwa huduma bora za vyoo zinaweza kusababisha mripuko wa magonjwa katika maeneo ya shule na nyumbani ambapo amewataka wataalamu wa afya wa kata na vijiji  kutembelea maeneo hayo ili kukagua na kuhimiza usafi wa mazingira  katika maeneo ya shule na makazi ya wananchi na kujikinga na mlipuko wa magonjwa hayo Huku kamati na bodi akizitaka kupeleka miundombinu ya maji kwa kushirikiana na wananchi ili vyoo  viweze kutumia maji.


Katika hatua nyingine Bi.Dumba amewataka wananchi kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na kwamba  hatua kali zinatakiwa kuchukuliwa kwa baadhi wanaoendekeza tabia hiyo ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa watoto huku akiwataka viongozi wa serikali za vijiji na kata kudhibiti tabia hiyo isiendelee kwani ni kitendo cha kumkandamiza mwanamke na mtoto.
 

MKURUGENZI WA HABARI ATOA UFAFANUZI TUZO YA JAJI WARIOBA

Na Magreth Kinabo, Maelezo
Mkurugenzi  wa Idara  ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene amesema Jaji Joseph Warioba alitunukiwa tuzo ya muungano iliyotukuka   kwa kuwa alistahili kupewa kama viongozi wengine na  kuwa kitendo si kumkejeli kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti  hivi karibuni.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  suala hilo katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika  kwenye Ukumbi wa  MAELEZO jijini Dares Salaam.
“Kumekuwa kuna taarifa katika baadhi ya magazeti kuwa Serikali kumpa tuzo Jaji Warioba ni kumkejeli, Ninapenda kuwataarifu kuwa  kitendo cha Serikali kumpa tuzo Jaji Warioba haikumkejeli wala kumtukana. Jaji Warioba anastahili kupewa tuzo kama mawaziri wakuu wengine kwa kuwa mchango wake katika muungano unajulikana,” alisema Mwambene. 
Tuzo hiyo aliyoipewa Jaji Warioba, wakati wa maadhimisho ya mika 50 ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar.
 Mwambene aliongeza kuwa  tuzo hiyo haihusiani na mjadala wa  Rasimu ya Katiba. Alifafanua kuwa katika mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Katiba uliokuwa ukifanyika katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, baadhi ya wajumbe walikuwa wanatoa mawazo yao na si kwamba wanapingana na Jaji Warioba. 
“ Mjumbe anatoa mawazo yake wakati wa kujadili  kwa kuwa hiyo bado ni rasimu, hivyo  hapingani  na Jaji Warioba,” alisisitiza huku akisema rasimu huwa inafanyiwa marekebisho.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo , alisema bado Ofisi yake inaendelea na hatua ya pili kuhusu gazeti la MAWIO kutoa maelezo ya kuchapisha habari yenye kichwa cha habari ‘Hati  Muungano Utata’.
Mwambene alifafanua kuwa ofisi hiyo inaendelea na suala hilo kwa hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa viongozi husika wa gazeti  kutoa maelezo baada ya hapo awali  kupeleka  barua ya kutaka maelezo hayo kwenye Ofisi za  gazeti la ‘MAWIO’ na kukuta zimefungwa.
 Aidha alisema kuwa hata majirani wa ofisi hizo walikataa kupokea barua hiyo, kwa maelezo kuwa kama ni masuala  ya habari  wahusika ndio wanapaswa kuipokea.
Aliongeza kwamba ofisi yake itafanya maamuzi sahihi ikiwahaitapata maelezo hayo, hivyo isijeikalaumiwa.
Mwambene aliwataka waandishi wa habari kuwa na kitambulisho  cha  uandishi wa habari (Press Card) na ametoa muda wa wiki moja kuanzia leo kwa mwandishi ambaye hana ili kuweza kukamilisha taratibu za kukipata.
Pia amewataka waandishi wa habari kuwa na heshima  katika utendaji kazi wa taaluma hiyo na kuzingatia mavazi yanayostahili kwani wao ni kioo cha jamii.

Lishe asili ni dawa ya wagonjwa wa moyo

140430034802_kula_vyakula_asili_inazidisha_miaka_ya_wagonjwa_wa_moyo_512x288_bbc_nocredit_c9f25.jpg
 Wanasayansi nchini Marekani wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.
Watafiti walichunguza zaidi ya watu elfu nne waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .
Vyakula ambayo havijapitia viwandani vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.CHANZO BBC