Tuesday, March 18, 2014

HOT NEWS: TAARIFA MUHIMU KUHUSU KUENDELEA KWA KIKAO CHA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO TAREHE 18 MACHI, 2014

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmYOiPgF1T3sMdwF20AVY0qnNohF_OErC0sICzmm3yXlHCa0G10oPB1PZyZJh2HUHSENRKE4CNTpRf0XKWCakkiMwwlKXu0TpEiohuQqZqUpAgir8YmVw_5D6JA76kUMBB4hBtyfcosSqG/s1600/unnamedj.jpgBaada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum kupelekea Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba  (pichani juu, akiongozwa kutoka Bungeni baada ya zoezi la kuwasilisha rasimu ya katiba kuahirishwa) kutokuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta aliitisha kikao cha maridhiano na baadhi ya wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali yaliyopo katika Bunge hilo ili kupata muafaka wa hoja zilizokuwa zimejitokeza.

Baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa manne na kumalizika saa nne za usiku, Mhe. Samuel Sitta amewaeleza waandishi wa Habari matokeo ya kikao hicho, ambapo wajumbe wa kamati hiyo wameafikiana yafuatayo:

Kikao cha Bunge Maalum kitaendelea leo tarehe 18 Machi, 2014 Saa tatu asubuhi kwa kuanza na shughuli za kuapisha baadhi ya wajumbe ambao hawakuapa awali kwa muda wa dakika 30 Kuhusu muda wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba, Wajumbe wameafikiana Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao kwa muda wa saa nne badala ya saa mbili alizokuwa ametengewa awali, ambapo uwasilishwaji wa rasimu huo utaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi baada ya shughuli ya viapo kumalizika.
 
Saa kumi kamili jioni kutakuwa na semina ya kanuni itakayofanyika katika Ukumbi wa Bunge ambapo Mwenyekiti wa iliyokuwa kamati ya kanuni Mhe. Prof. Costa Mahalu na wenzeke watawawezesha wajumbe kupitia vifungu vya kanuni hizo za Bunge Maalum, ambapo semina hiyo itaendelea hadi jumatano tarehe 19 machi, 2014 Siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi, kutakuwa na semina itakayoendeshwa na maafisa wawili kutoka kenya ambao watatoa uzoefu wao katika maeneo haya.
 
Aidha wajumbe wamekubaliana Mhe. Rais kulihutubia Bunge siku ya Ijumaa jioni kama ilivyokuwa imepangwa awali, ambapo asubuhi kutatanguliwa na shughuli za Mwenyekiti wa Bunge Maalumu kuunda kamati 14 za Bunge Maalum.


 News alert hii imeletwa na 

Owen Mwandumbya Kutoka Sekretariet ya Bunge Maalum
Categories:

No comments:

Post a Comment