Sunday, May 4, 2014
MAADHIMISHO YA SIKU YA ALBINO DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DAR
Na Waandishi Wetu
Maadhimisho ya Siku ya Albino Duniani yamefanyika leo katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wakitaifa na kimataifa.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo yaliyokuwa yanafikia kilele leo
alikuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete
yalihudhuriwa pia na Balozi wa Uturuki nchini Hon. Ali Dovutoglu.
Pamoja na shamrashamra nyingine maadhimisho hayo yaliambatana na
huduma za afya kama upimaji wa kansa ya ngozi na macho kwa albino
zilizotolewa bure kuendana na kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo: HAKI YA AFYA, HAKI YA UHAI.
(Picha: Chande Abdallah na Shani Ramadhani /GPL)
Subscribe to:
Posts (Atom)